BIMA YA USAFIRISHAJI MIZIGO YA NDANI YA NCHI

Bima ya usafirishaji mizigo ya ndani ya nchi ni ipi?

Hii ni bima inayokinga mzigo /bidhaa uliyobeba wakati wa usafirishaji ndani ya nchi kwa njia ya barabara, maji, reli au hata anga. Bima hii inakukinga na uharibifuwa mzigo ambao unaoweza kusababishwa na binadam au ajali itokanayo na majanga ya asili. Bima hii pia inaweza kutoa kinga kwa wahusika wengine  watakao husika wakati wa kupakia au kupakua  mizigo na mara nyingi kinga hii  hutumika kwa usafiri wa reli na barabara. Kama unatumia njia ya maji au anga basi itakupasa upate bima ya mizigo ya aina nyingine (Marine cargo insurance) ili uweze kuwa na kipengele hiki kinachokinga mali yako wakati wa kupakia na kupakua.  

Bima hii huanza mara tu mizigo yako inapopakiwa kwenye chombo cha usafiri na kuisha  pale mizigo yako inaposhushwa mwisho wa safari. Iwapo itatokea bahati mbaya na mzigo wako usifike mahala husika kutokana na shida iliyojitokeza bima hii itaendelea kukukinga hata pale mzigo wako utakaposhushwa na kupakiwa kwenye chumba kingine cha usafirishaji . 

Bima ya usafirishaji wa mizigo ya ndani wakati  mwingine hufananishwa na kuchanganywa na Bima ya mizigo (Marine cargo ) sababu ya kufanana kwake katika kutoa kinga ya mizigo yako wakati wa usafirishaji wake. Ukitaka kuielewa zaidi bima hii bonyeza hapa kupata maelezo zaidi  Bima ya mizigo 

Nani anatakiwa kukata bima hii ya usafirishaji wa mizigo ya ndani ya nchi?

Bima hii inapatikana kwa watu binafsi ,mashirika na  taasisi mbalimbali na ni mhimu kama utakata bima pindi unapotaka kusafirisha mizigo au bidhaa yako. 

Bima yetu itakupa kinga kwa kuzingatia yafuatayo.;

  • Iwapo unatumia lory au gari ambalo unalimiliki au kumilikiwa na kampuni , gari hilo ni mhimu liwe limetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kubeba mizigo .
  • Iwapo utakuwa unatumia gari, au lori la kukodi kwa ajiri yako au shirika lako.

Bima ya usafirishaji mizigo ndani ya nchi inakulinda dhidi ya yafuatayo:

  • Wizi wa mizigo wakati ikiwa safarini.
  • Uharibifu wa mali uliosababishwa na ajali wakati wa usafirishaji. 
  • Upotevu wa mali wakati wa usafirishaji
  • Moto
  • Radi 
  • Kuvunjika kwa daraja 
  • Kugongana na gari jingine 
  • Kupinduka kwa gari lako la mizigo. 
  • Iwapo train ya mizigo itahama kwenye reli na kupata ajali.

Unaweza kuchagua aina ya bima unayotaka kutoka kwenye maelezo hapo chini:

  1. Bima ya wazi hii ni ile ambayo yakupasa uoneshe na useme usafirishaji mizigo wote unazotarajia kuzifanya ndani ya mwaka 
  2. Bima ya  kwa ajili ya safari mahsusi.  Hii ni maalum kwa safari moja ya usafirishaji wa mizigo ambayo inakatatwa kabla ya safari hiyo husika . 

Ni kitu gani kingine unatakiwa kujua kuhusu bima hii?

Sera yetu huenda mbali na kulinda gharama zinazoweza kujitokeza kutokana na

  • Gharama ya kuondoa mabaki ya mali au mzigo kutoka mahali yalipoharibikia 
  • Kuhamisha mzigo kutoka eneo la ajali  na kuupakia kwenye usafiri mwingine.
  • Kuulinda mzigo katika eneo la ajali.
  • Kuharibika kwa vifaa vya kubebea mizigo kutokana na ajali. 

Ni mhimu kujua ya kwamba kiasi  kitakacholipwa hapa kitahusisha na kufuata sera yetu ya ukomo . Hivyo kiasi chochote kitakacholipwa kwa madai hakitazidi  kiasi kilichotajwa kwenye sera yetu.

Kwa kuwa umeshajifunza kuhusu bima hii tafadhali bonyeza hapa kwa manunuzi ya bima hii au tupigie kwenye +255222774999, 2775039 au omba kupigiwa kwa ku bonyeza hapa . 

 

Kindly note that client login is only available to existing ICEA LION customers
Click here to proceed to the Self Service Portal if you are already a client of ICEA LION.
Otherwise, see products available to buy online