Bima ya makazi ni bima inayokupa ulinzi dhidi ya hasara inayoweza kuletwa na majanga kwenye nyumba au vilivyomo ndani ya nyumba yako. Bima hii inaweza kuongezwa na kuhusisha vitu/vifaa vingine kama simu, mikufu ya thamani na hata wafanyakazi wa ndani .Ni mhimu kujua kwamba unaweza kupata bima hii kama mmiliki wa nyumba au hata mpangaji ndio maana bima hii huitwa ‘Domestic package” kutokana na ukweli kwamba bima hii haiishii kwenye kinga dhidi ya jingo tu bali kwa kila kitu kinachopatikana ndani ya nyumba husika.
Faida ya kuwa na Bima hii ya makazi:
Iwapo utataka kuwasiliana na sisi tafadhali tupigie +255 22 277 4999, +255 22 277 5039 au omba kupigiwa kwa ku bonyeza hapa
Ingiza maelezo yako ili tuweze kupanga simu kwa ajili yako
Bima yetu ya nyumba imegawanyika katika vipengele tofauti ili kukuwezesha kukata bima kwa kile tu unachotaka kukikinga . Kwa mfano huitajiki kukata bima ya jingo kama wewe ni mpangaji, Hapa bima utakayokata ni ile ya samani,vifaa vya ndani , vito vya thamani nk.
Hii ni bima inayokatwa kwa ajili ya jengo ambapo mkataji ni yule mmiliki wa jengo.
Hii ni Bima ya vifaa/vitu vya ndani vya mmiliki wa nyumba au hata mpangaji . Vitu hivyo ni kama samani za ndani,vifaa vya umeme, mapambo ya ndani na vitu vingine vinavyohamishika. Pia unaweza kukatia bima vitu/vifaa vinavyopatikana kwenye karakana yako au kwenye nyumba ndogo ya mtumishi. Ingawa yakupasa kutoa taarifa sahihi wakati wa kukata bima hii.
Hii ni bima inayokatwa kwa ajili ya mali au vifaa vyote ambavyo havijahusika au kutajwa kwenye kipengele A & B hapo juu. Vifaa/Vitu vinavyohusika katika katika kipengele hiki ni pamoja na vito vya thamani , saa, dhahabu,madini ya fedha, picha za thamani, nguo, miwani , na mizigo au vifurushi vya matumizi binafsi . Ni mhimu kujua kuwa iwapo utapoteza kitu/kifaa ambacho hukukitolea maelezo ya bei na thamani yake utalipwa kiasi kisichozidi 100000/=Tshs kama fidia . Mfano iwapo utaleta madai dhidi ya kuibiwa au kuharibika kwa miwani kutokana na majanga na haukuonesha wala kueleza thamani ya miwani hiyo hapo awali utafidiwa kwa kiasi kilichotajwa yaani kisichozidi 100,000/=Tsh.
Hii ni bima ambayo inakinga dhidi ya matatizo yanayoweza kutokea kwa mfanyakazi wa ndani kama kifo,majeraha .magonjwa yaliyojitokeza wakati mfanyakazi huyo akiwa katika majukumu yake ya kila siku .wafanyakazi hawa ni kama dereva, mlinzi, mpishi na mtunza bustani.
Hii ni bima inayokatwa na mwajiri kujikinga dhidi ya mashitaka yoyote ya kisheria yanayoweza kuletwa na mfanyakazi wa ndani kutokana na ajali, magonjwa,kifo majeraha yaliyotokea akiwa katika majukumu ya kazi.
Kipengele hiki kina mkinga mmiliki wa jengo dhidi ya mashtaka au madai yanayoweza kuletwa na mtu wa tatu . Mtu wa tatu anayetajwa hapa ni yule ambaye sio sehemu ya familia au watu unaoishi nao au watu wanaofanya kazi nyumbani kwako. Bima hii inakulinda iwapo utashitakiwa na mtu wa tatu kwa sababu ya kifo ,majeraha au ugonjwa uliosababishwa na ajali kwenye jengo lako .
Kipengele hiki kinakulinda wewe mkazi pamoja na wafanyakazi,au watu wanaoishi ndani ya nyumba yako dhidi ya mashtaka yanayoweza kuletwa dhidi ya janga lililotokea katika makazi yako na kusababisha madhara dhidi ya watu wengine tofauti na wakazi rasimi katika nyumba yako . Iwapo mfaidika wa dai hili atakuwa amefariki malipo haya yatalipwa kwa muwakilishi wa mfaidika kwa mujibu wa sheria.
Tembelea msingi wetu wa Maarifa
Huduma ya zima moto: ICEA LION watakulipa fidia ya gharama za zima moto
Tujulishe iwapo umeshitakiwa: iwapo una bima dhidi ya mashitaka kama zilivyoainishwa kwenye vipengele D hadi G hapo juu tujulishe kwa ajili ya msaada wa kisheria . tutakusaidia katika kulipa fidia pamoja na gharama za kesi ya kumshitaki yeyote anayeweza kuwa amehusika pia.
Janga likitokea wakati nyumba/makazi hayakaliwi na mtu: ICEALION haitalipa madai yeyote iwapo janga litatokea kwenye nyumba/jengo ambalo hakuna mtu ameishi au kukaa ndani yake ndani ya siku 30.
Uharibifu wa makusudi utakaotendwa na wanafamilia au wafanyakazi wa ndani hautalipwa
Fedha & Nyaraka hazihusiki: Bima yetu ya Makazi/nyumba haikingi dhidi ya vitu kama hati,Ankara, fedha, machapisho, medali, gari,, vifaa vya gari, isipokuwa kama kulikuwa na makubaliano ya kuvikatia bima vitu hivyo..
Vifaa vinavyohamishika ni lazima viwepo na mmiliki wakati janga linatokea : mhimu kujua ya kwamba ICEA LION haitafanya malipo ya madai kwa vifaa ulivyovikatia bima kwenye kipengele C iwapo vitu au mali hizo zimepotea au kuharibiwa na janga ukiwa safarini. Malipo yatafanywa tu endapo utakuwa ndani ya nchi na sehemu uliyoitaja kama makazi yako rasimi . ukitaka kuwa na bima ya mali/vifaa vyako wakati ukiwa safarini tunakushauri ukate bima ya safari. Bonyeza hapa kupata bima ya safari ndani ya dakika moja.
Hatari ya vitu vinavyolipuka : Iwapo unahifadhi vitu kama mafuta au vitu vingine vinavyoweza kulipuka na kusababisha ajali ICEALION haitakulipa madai hayo.
Head Office
Plot 331 Kambarage (Rose Garden road) Road, Mikocheni
P.O. Box 1948 Dar Es Salaam
Tel: +255 22 2774999, +255 22 2775039, +255 22 2775059
Fax: +255 22 2775094
E-Mail: insurance@icealion.co.tz
Website: www.icealion.co.tz
Something isn’t Clear?
If you would like to talk to us in person, you can call us on +255 22 277 4999, +255 22 277 5039 or request a call back by clicking here.