BIMA YA NYUMBA/MAKAZI 

Bima ya Makazi/Nyumba ni ipi?

Bima ya makazi ni bima inayokupa ulinzi dhidi ya  hasara inayoweza kuletwa na majanga kwenye nyumba au vilivyomo  ndani ya nyumba yako. Bima hii inaweza kuongezwa na kuhusisha vitu/vifaa vingine kama simu, mikufu ya thamani na  hata wafanyakazi wa ndani .Ni mhimu kujua kwamba unaweza kupata bima hii  kama  mmiliki wa nyumba au hata mpangaji  ndio maana bima hii huitwa ‘Domestic package” kutokana na ukweli kwamba bima hii haiishii kwenye kinga dhidi ya jingo tu bali kwa kila kitu kinachopatikana ndani ya nyumba husika. 

Faida ya kuwa na Bima hii ya makazi:

  • Utalipwa fidia dhidi ya hasara itakayosababishwa na Moto, tetemeko la ardhi, kimbunga na  mafuriko.
  • Utalipwa fidia dhidi ya hasara iliyosababishwa na Milipuko itokanayo na shughuli za nyumbani
  • Utalipwa fidia dhidi ya Madhara yanayoweza kuletwa na ghasia au vurugu za kiraia, kidini au kikabila,
  • Utalipwa fidia dhidi ya hasara iliyosababishwa na Kupasuka kwa mabomba na matanki ya maji.
  • Utalipwa fidia dhidi ya hasara iliyosababishwa na Wizi wa mali.
  • Utalipwa fidia dhidi ya Madhara yanayoweza kujitokeza baada ya ndege kuanguka au kitu chochote kutoka angani mfano kimondo.

Ni Vitu gani vya msingi katika bima ya nyumba/makazi? 

Bima yetu ya nyumba imegawanyika katika  vipengele tofauti ili kukuwezesha kukata bima kwa kile tu unachotaka kukikinga . Kwa mfano huitajiki kukata bima ya jingo kama wewe ni mpangaji, Hapa bima utakayokata ni ile ya  samani,vifaa vya ndani , vito vya thamani  nk. 

Kipengele A: Jengo 

Hii ni bima inayokatwa kwa ajili ya jengo ambapo mkataji ni yule mmiliki wa jengo,

Bima hii inahusisha upotevu au uharibifu kwenye jengo kama ifuatavyo:

  • Upotevu au uharibifu wa  vifaa kama milango, viyoyozi , ukuta , mageti , karakana na vinginevyo kutokana na majanga yaliyoanishwa hapo juu,
  • Gharama zilizojitokeza kutokana na kutafuta makazi na malazi mbadala iwapo janga litasababisha nyumba kuwa haifai kwa matumizi kwa mda huo. 
  • Kulipwa kwa fidia kwa mmiliki wa jengo ambaye hajalipwa kodi na mpangaji kutokana na jengo hilo kupatwa na majanga. Kiwango kitakacholipwa  ni kile ambacho hakivuki  10% ya  kiasi cha thamani ya jengo. 
  • Ni mhimu kujua kwamba kiasi kitakacholipwa hakitakiwi kuzidi 10% ya kiasi cha thamani ya nyumba/jengo 

Kipengele B: Vifaa & Vitu  vya ndani 

Hii ni Bima ya vifaa/vitu vya ndani vya mmiliki wa nyumba au hata mpangaji . Vitu hivyo ni kama samani za ndani,vifaa vya umeme, mapambo ya ndani na vitu vingine vinavyohamishika. Pia unaweza kukatia bima vitu/vifaa vinavyopatikana kwenye karakana yako au kwenye nyumba ndogo ya mtumishi. Ingawa yakupasa kutoa taarifa sahihi wakati wa kukata bima hii.

Kipengele C: Bima ya vifaa vyote.

Hii ni bima inayokatwa kwa ajili ya mali au vifaa vyote ambavyo havijahusika au kutajwa kwenye kipengele A & B hapo juu. 

Vifaa/Vitu vinavyohusika katika katika kipengele hiki ni pamoja na vito vya thamani , saa, dhahabu,madini ya fedha, picha za thamani, nguo, miwani  , na mizigo au vifurushi vya matumizi binafsi . Ni mhimu kujua kuwa iwapo utapoteza kitu/kifaa ambacho hukukitolea maelezo ya bei na thamani yake utalipwa kiasi kisichozidi 100000/=Tshs kama fidia . Mfano iwapo utaleta madai dhidi ya kuibiwa au kuharibika kwa miwani kutokana na majanga na haukuonesha wala kueleza thamani ya miwani hiyo hapo awali utafidiwa kwa kiasi kilichotajwa yaani kisichozidi 100,000/=Tsh.

Ni mhimu kujua kwamba kuharibika  kwa kifaa/kitu kulikosababishwa na kuisha kwa matumizi, kushuka thamani, kupatwa na kutu, kuharibika kwa sababu za asili, kifaa/mali kutaifishwa au kufilisiwa na serikali au kuibiwa na mmoja ya wana familia hakutakuwa na ustahili wa kulipwa fidia yeyote.

 Kipengele D: Wafanyakazi wa ndani

Hii ni bima ambayo inakinga dhidi ya matatizo yanayoweza kutokea kwa mfanyakazi wa ndani kama kifo,majeraha .magonjwa  yaliyojitokeza wakati mfanyakazi huyo akiwa katika majukumu yake ya kila siku .wafanyakazi hawa ni kama dereva, mlinzi, mpishi na mtunza bustani.

Fidia zitolewazo katika kipengele hiki ni kama ifuatavyo: 

  • Kifo cha mfanyakazi – Fidia ni mshahara wa miezi 
  • Madai ya matibabu – ni 2,000,000/= kwa kila dai
  • Gharama ya mazishi  – ni 600,000/= kwa kila mfanyakazi

Ni mhimu kujua kwamba madai yako yanatakiwa kuwa yanazidi kiasi cha shilingi 100.000/= isipokuwa kwa madai ya gharama ya mazishi.

Kipengele E: Kinga ya Muajiri. 

Hii ni bima inayokatwa na mwajiri kujikinga dhidi ya mashitaka yoyote ya kisheria yanayoweza kuletwa na mfanyakazi wa ndani kutokana na ajali, magonjwa,kifo majeraha yaliyotokea akiwa katika majukumu ya kazi.

Bima hii itamlipa mdai/mlalamikaji kwa kuzingatia ukomo wa kiasi kama ifuatavyo:

  • Mtu mmoja shilling 50,000,000/=
  • Kwa kila tukio – shilingi 250,000,000/-
  • Ndani ya Mwaka -shilingi 500,0000,000/-

Ni mhimu kutambua ya kwamba  kiasi cha shilingi 5,000,000/= kitapunguzwa kwa kila dai kama mchango wa mteja kwenye janga hilo.

Iwapo mfaidika wa dai hili  atakuwa amefariki malipo haya yatalipwa kwa muwakilishi wa mfaidika kwa mujibu wa sheria.

Kipengele F: Kinga ya mmiliki

Kipengele hiki kina mkinga mmiliki wa jengo dhidi ya mashtaka au madai yanayoweza kuletwa na mtu wa tatu . Mtu wa tatu anayetajwa hapa ni yule ambaye sio sehemu ya familia au watu unaoishi nao au watu wanaofanya kazi nyumbani kwako. Bima hii inakulinda iwapo utashitakiwa na mtu wa tatu kwa sababu ya kifo ,majeraha au ugonjwa uliosababishwa na ajali kwenye jengo lako .

Kipengele  G: Kinga ya mkazi   &  na mtu binafsi.

Kipengele hiki kinakulinda wewe mkazi pamoja na wafanyakazi,au watu wanaoishi ndani ya nyumba yako dhidi ya  mashtaka yanayoweza kuletwa dhidi ya janga lililotokea katika makazi yako na kusababisha madhara dhidi ya watu wengine tofauti na wakazi rasimi katika nyumba yako .

Iwapo mfaidika wa dai hili  atakuwa amefariki malipo haya yatalipwa kwa muwakilishi wa mfaidika kwa mujibu wa sheria.

Ni kitu gani kingine nahitaji kujua kuhusu bima hii ya nyumba/makazi?

  • Huduma ya zima moto: ICEA LION watakulipa fidia ya gharama za zima moto  
  • Tujulishe iwapo umeshitakiwa:  iwapo  una bima dhidi ya mashitaka kama zilivyoainishwa kwenye vipengele D hadi G hapo juu tujulishe kwa ajili ya msaada wa kisheria . tutakusaidia katika kulipa fidia pamoja na gharama za kesi ya kumshitaki yeyote anayeweza kuwa amehusika pia.
  • Uharibifu wa makusudi utakaotendwa na wanafamilia au wafanyakazi wa ndani hautalipwa
  • Janga likitokea wakati nyumba/makazi hayakaliwi na mtu:  ICEALION haitalipa madai yeyote iwapo janga litatokea kwenye nyumba/jengo ambalo hakuna mtu ameishi au kukaa ndani yake ndani ya siku 30.
  • Fedha  & Nyaraka  hazihusiki:  Bima yetu ya Makazi/nyumba haikingi dhidi ya vitu kama hati,Ankara, fedha, machapisho, medali, gari,, vifaa vya gari, isipokuwa kama kulikuwa na makubaliano ya kuvikatia bima vitu hivyo..
  • Vifaa vinavyohamishika ni lazima viwepo na mmiliki wakati janga linatokea :  mhimu kujua ya kwamba  ICEA LION haitafanya malipo ya madai kwa vifaa ulivyovikatia bima kwenye kipengele  C iwapo vitu au mali hizo zimepotea au kuharibiwa na janga  ukiwa safarini. Malipo yatafanywa tu endapo utakuwa ndani ya nchi na sehemu uliyoitaja kama makazi yako rasimi . ukitaka kuwa na bima ya mali/vifaa vyako wakati ukiwa safarini tunakushauri ukate bima ya safari. Bonyeza hapa kupata bima ya safari ndani ya dakika moja.
  • Hatari ya vitu vinavyolipuka : Iwapo unahifadhi vitu kama mafuta au vitu vingine  vinavyoweza kulipuka na kusababisha ajali ICEALION haitakulipa madai hayo. 
  • Kwakua umeelewa bima yetu ya MAKAZI/NYUMBA karibu upate bima yako kwa ku Bonyeza hapa. Iwapo utataka kuwasiliana na sisi tafadhali tupigie +255 22 277 4999, +255 22 277 5039 au omba kupigiwa kwa ku bonyeza hapa  

 

Kindly note that client login is only available to existing ICEA LION customers
Click here to proceed to the Self Service Portal if you are already a client of ICEA LION.
Otherwise, see products available to buy online