BIMA YA MIZIGO
Hii ni bima ya mizigo inayokulinda dhidi ya hasara au uharibifu utakaotokea kwa bidhaa zako zikiwa njiani kutoka kwa muuzaji kuja kwako. Mzigo huu utasafirishwa kwa njia ya maji ingawa sera yetu inaweza pia kulinda mzigo wako wakati ukisafirishwa kwenda au kutoka bandari kwa kupitia barabara, reli, anaga au hata njia za maji zilizopo ndani ya nchi. Pia tuna uwezo wa kukukatia bima itakayokulinda kutoka sehemu ulipotolewa mzigo mpaka mahala mzigo utakapohifadhiwa . Bima hii hujulikana kama Bohari kwa Bohari (warehouse to warehouse)
Kwa ujumla , tunakulinda dhidi ya hasara au uharibifu wowote utakaotokea kwenye mizigo au shida yoyote itakayotokea wakati wa usafirishaji.. Unaweza kununua bima yetu ya mizigo kwa njia ya hapa.
Mhimu: Pia tunatoa bima inayotoa kinga dhidi ya chombo cha usafiri majini Marine Hull Insurance. Hii ni bima inayokatwa maalumu kwa ajili ya chombo chako (Meli) ,bima hii haihusishi injini ya meli na baadhi ya vifaa ambatanishi kama masts, na rigging . Kujua zaidi kuhusu bima hii bonyeza hapa
Ni tatizo gani linaweza kutokea wakati mzigo wako ukisafirishwa majini?
Kuna matukio kadhaa yanayoweza kuathiri ufikishwaji wa mzigo wako wakati wa usafirishwaji kwa njia ya maji kama ifuatavyo:
Majanga ya baharini: Haya ni yale majanga ya asili yanayoweza kutokea baharini ambayo binadaamu hawezi kuyazuia . majanga haya ni kama kimbunga, radi, tetemeko, kuzama kwa meli, kugongana , kupotea kwa meli, nakadhalika. Ijulikane ya kwamba majanga ya baharini hayahusishi kila ajali au majeruhi . majeruhi waliotokana na kuharibika kwa kawaida kwa meli, matukio ya kujitakia ,au kushindwa kuelekeza vizuri timu ya wataalam wa meli. Inagawa pia majanga ya baharini ni pamoja na kupotea kabisa kwa mizigo yako, kuingia kwa maji kwenye meli, kuzama au kukwama kw meli..Pia inahusisha jettison ambalo ni neno la kitaalam linalomaanisha kudondosha au kuondoa mizigo kutoka kwenye ndege au meli kwa ajili ya kuokoa meli isizame. Hapa patatumika sheria ya Law of general coverage ambayo ni kanuni ya ubaharia ambapo wadau wote hugawana hasara iliyopatikana kutokana na maamuzi ya kimakusudi yaliyofanyika kupunguza mizigo kwenye meli ili kuokoa mizigo itakayobaki. Kutokana na dharura kama
- Moto au kulipuka kwa meli
- Meli kugangana na meli nyingine
- Vita, ugaidi, machafuko
- Ujambazi wa baharini
- Majanga ya asili kama tetemeko , sunami, milipuko ya volkano, na mengine
- Sababu za kibinadamu : upakiaji mbaya wa mizigo, upakuaji mbaya wa mizigo, kutumia watu wasio na utaalamu au barratry ambayo ni makosa yanayofanywa na kiongozi wa msafara yatakayopelekea kuharibu mzigi au chombo chenyewe.
- Majanga yasababishwayo na binaadam: majanga haya ni kama wizi ,kutekwa, vita na mengineyo.
Ni bima ipi ya mizigo inayosafirishwa na meli inapatikana ICEA LION
Bima za meli na mizigo huwa zinafuata utaratibu uliokubalika na Institute Cargo Clauses (ICC) hawa ndio wanaotoa mwongozo sahihi wa ni kipi kinachokatiwa bima na kipi kitalipwa iwapo patatokea uharibifu au upotevu wa mali.
Kuna vifungu vya aina tatu vya Bima za usafirishaji wa mizigo kwa njia ya maji
- Kifungu A:(Institute Cargo Clauses ICC(A) All Risks): Hiki ndio kifungu kipana chenye kuchukua majanga yote yasababishayo uharibifu au upotevu wa mali isipokuwa yale tu yaliyotengwa kwa mujibu wa makubaliano.
- Kifungu B: (Institute Cargo Clause ICC(B): Hiki ni kifungu ambacho hukinga dhidi ya majanga maalumu ambayo mteja ametaka kujikinga nayo. Kifungu hiki hutoa bima ile ya msingi na kuacha vitu vingine vinavyopatikana kwenye kifungu.
- Kifungu C: Institute Cargo Clause(C): Hiki ni kifungu ambacho bima inatoa kinga kwa majanga yaliyochaguliwa pekee.
Ni mhimu kujua kwamba vifungu vyote vilivyotajwa hapo juu vinahusisha bima ya bidhaa au mizigo ambayo iko katika safari .
Bima ya usafirishaji kwa njia ya Maji inatoa kinga dhidi ya:
- Upotevu wa mizigo wakati wa kusafirishwa.
- Uharibifu wa mzigo wakati wa usafirishaji.
- Kuibiwa kwa sehemu ndogo ya mzigo
- Wizi wa mzigo wote wakati wa usafirishaji
- Kuharibika kwa bidhaa kutokana na kuchanganyika na maji, unyevu, mafuta au madawa
- Kushindwa kuwasilisha mzigo katika sehemu ya mwisho.
Ni kipi hakipo katika Bima ya usafiridhaji wa mizigo kwa njia ya maji.
- Hasara inayotokea kutokana na mteja kushindwa kusema ukweli wa bidhaa halisi alizobeba, umri wa meli nk . Au kufanya madai yenye lengo la kufanya utapeli ili kujipatia fedha.
- Kuvuja kwa chombo, au mali au mzigo kupoteza uzito au ujazo au kuchoka na kuharibika kwa mzigo katika hali ya kawaida (ambayo haijasababishwa na majanga
- Upotevu au uharibifu wa mzigo kutokana na matayarisho au njia mbaya za upangaji mizigo.
- Chombo/kontena kutokuwa na umadhubuti au ubora unaostahili.
- Hasara ambayo mteja anaweza kutegemea itatokea kutokana na aina ya mzigo. Hii kwa kitaalam inaitwa inherent vice of the subject matter. Kwa mfano iwapo utakuwa unataka usafirishe matunda kama parachichi na safari ikachelewa basi bima yetu haitalipa fidia ya hasara itakayojitokeza
- Hasara au uharibifu utakaojitokeza kutokana na kukawia kwa safari .
- Vita na machafuko . unaweza kulipia kiasi cha ziada ili kujikinga na madhara yanavyoweza kuletwa na vita au machafuko wakati wa safari.
- Majanga yanayohusiana na mashambulizi na ugaidi.
- Vitu vingine kama vilivyoainishwa kwenye sera yetu.
Ni taarifa zipi zinahitajika ukitaka kupata bima ya usafirishaji mizigo kwa njia ya maji.
- Maelezo ya bidhaa/mzigo , idadi na aina ya mzigo.
- Thamani halisi ya mzigo.
- Maelezo ya chombo cha usafirishaji .
- Maelezo ya safari nzima ambako chombo kitapita.
- Fomu yenye orodha ya vitu vilivyomo katika mzigo wako.
- Aina ya kifungu cha bima unayotaka kukata. Mfano . ICC (A), (B), (C)
- Ankara ya malipo
Kuna mengi ya kujifunza juu ya bima hii tafadhali bonyeza kwenye maelezo yaliyopo chini:
- Thamani halisi ya mzigo utakaokatiwa bima
- Nifanye nini nikigundua upotevu au uharibifu wa mizigo yangu.
- Ni nyaraka gani zinatakiwa wakati wa kufungua madai.
- Ni nini kingine kitakingwa na bima hii iwapo ntalipa kiasi cha ziada.
- Bima ya Meli ni nini?
- Nani anahusika na kukata bima kwenye vipengele tofauti vya safari.
- Gharama ya mzigo ukiwa umefika kwenye meli kabla ya kusafiri. (FoB)?
- Gharama za mzigo na nauli yake ni nini? Cost & Freight (C&F)
- Gharama ya bima na usafirishaji ni nini? Cost Insurance & Freight (CIF)
- Najuaje kuwa kitu kipi na kwa gharama gani ntakatia bima
- Thamani halisi ya mali ni nini?
- Ni vitu gani vinaweza kuathiri gharama ya Bima ?
- Ni vitu gani vya kuzingatia katika kuweka gharama.?
- Bima ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya maji ni nini?
- Bima ya usafirishaji wa majini iliyo wazi ni ipi?
- Nini maana ya Bohari kwa Bohari ?
- Kifungu cha vita ni kipi? Institute War Clauses – Cargo (ICC)?
- Kifungu cha shambulizi ni kipi? – Institute Strikes Clauses?
- Je bidhaa hulindwa na bima mda wote wa safari?
- Ankara ya upakiaji mizigo ni nini?
- Haki ya bima ni nini?
- Uaminifu katika bima ni nini?
- Nini hutokea iwapo nitaweka thamani ndogo ya mzigo ili nisilipie bima kubwa.
Kwa kuwa umeshajifunza kuhusu bima hii tafadhali bonyeza hapa kwa manunuzi ya bima hii au tupigie kwenye +255222774999, 2775039 au omba kupigiwa kwa ku bonyeza hapa.

