BIMA YA KINGA YA MUAJIRI 

Bima ya Kinga ya muajiri ni ipi?

Hii ni bima inayokatwa na muajiri kujikinga dhidi ya mashitaka yoyote ya kisheria yanayoweza kuletwa na mfanyakazi wake kutokana na ajali, magonjwa,kifo au majeraha yaliyotokea akiwa katika majukumu ya kazi. Iwapo muajiri binafsi kwa bahati mbaya atafariki kipengele hiki kitaendelea kumkinga muwakilishi wa muajiri kama mke/mume au muwakilishi wa familia iwapo yatafunguliwa mashtaka na mtu wa tatu. Kwa upande wa kampuni kinga hii huikinga kampuni iliyotoa ajira dhidi ya mashtaka yeyote yanayoweza kuikabili  kampuni au hasara za kiuchumi zitakazo sababishwa na mfanyakazi wake aliyepata majanga.

Bima hii itakulipa wewe muajiri fidia ya hasara iliyojitokeza kutokana na kifo na gharama za kisheria kwa ukomo wa sera yetu. Sera yetu ya bima hii itakuonesha mipaka na ukomo wa kiasi cha fedha unachopaswa kulipwa kwa  kila mfanyakazi na kwa kila tukio.

Ni nani anahitaji bima hii ya kinga ya Muajiri?

Bima hii inamfaa muajiri yeyote ambaye anatafuta kinga dhidi ya hasara ya kiuchumi inayoweza kuletwa na majeraha, magonjwa , au kifo cha mfanyakazi wakati akiwa katika shughuli zake za majukumu ya kikazi. 

Ni kitu gani hakihusiki kwenye Bima hii?

Kuna baadhi ya mambo ambayo hayahusiki kwenye sera ya bima yetu na ni mhimu kujua ya kwamba  huwezi kuyafungulia madai: 

  • Ajali yeyote itakayo sababisha kifo au majeraha ambayo imetokea nje ya muda wa kazi wa muajiri wako haitalipwa fidia.
  • Majeraha ya ajali au ugonjwa uliopatikana nje  ya mipaka ya ya kikazi  kwa muajiriwa ambaye mkataba wake wa kikazi haujafanywa Tanzania na haufati sheria za nchi ya Tanzania .

Kwa kua sasa umeelewa bima ya kinga ya muajiri ni nini na ungependa kukata bima hii . tafadhali bonyeza hapa ili uweze kupigiwa au tupigie  +25522277499 

Kindly note that client login is only available to existing ICEA LION customers
Click here to proceed to the Self Service Portal if you are already a client of ICEA LION.
Otherwise, see products available to buy online