BIMA YA GARI BINAFSI

Bima ya Gari ni nini?

Hii ni bima inayokulinda dhidi ya hasara unayoweza kuipata kiuchumi  iwapo chombo chako, vipuri  na vifaa vitaibiwa au kuharibika kutokana na ajali, moto au vurugu. Bima hii pia hukulinda dhidi ya madhara unayoweza kusababisha kwa mtu wa tatu 

ICEA LION inatoa Bima ya Magari ya biashara na magari binafs.,Bima binafsi ina vipengele vitatu navyo ni: bima ndogo pekee, bima ndogo ya wizi na moto na bima kubwa..Bonyeza hapa kujifunza zaidi.

Tovuti yetu inaakuwewezesha kupata bei , kununua na kupata cheti au stika yako itakayotumwa kwako kwa njia ya barua pepe papo hapo. Bonyeza hapa kupata huduma yetu kwa haraka. 

Kwanini ni mhimu kuwa na bima ya gari?

  • Ili uweze kuendesha gari lako katika  Barabara za nchini Tanzania ni lazima na kwa mujibu wa sheria ya bima ya Mwaka 2002 (Insurance Act,169 Cap revision edition of 2002)  uwe umekatia bima ndogo gari lako. 
  • Bima inakuhakikishia kulipwa fidia aukutengenezewa gari  pindi unapopata hasara ya kuibiwa au kuharibiwa kwa chombo chako kutokana na ajali. 

Ni mambo gani yapo kwenye Bima kubwa  

Iwapo utaamua kuchukua  Bima kubwa italipwa fidia kwa mambo yafuatayo::

  • Iwapo chombo chako, vipuri na vifaa vitaibiwa au kuharibika kutokana na ajali, moto au vurugu.)
  • Iwapo kutatokea kifo cha aliyekuwa akitumia gari (mtu mwingine) na mtu/watu wengine waliohusika na ajali hiyo (ambao hawakuwa kwenye gari lako))
  • Iwapo kutakuwa na gharama za matibabu kutokana na ajali
  • Iwapo gari lako litagonga na kuharibu mali ya mtu mwingine.
  • Iwapo gari litaibiwa au kuharibiwa likiwa katika uangalizi wa karakana/gereji
  • Iwapo utasababisha majeraha kwa mtu mwingine na akahitaji huduma au msaada wa matibabu ya dharura unaruhudiwa kumpeleka hospitali na kumpa matibabu yenye gaharama mpaka ya shilingi 500,000/= kiasi hiki cha fedha kitarudishwa kwako na ICEA LIONbaada ya kuwasilisha nyaraka kutoka hospitalini ikiwa ni pamoja na ripoti ya daktari na stakabadhi. 
  • Iwapo kioo cha mbele cha gari yako kitavunjika au kuharibika utalipwa kati ya 500,000/- hadi 1,000,000/- kwa kutegemea na aina ya gari lako. Gharama hizi zitafanyiwa tathimini na iwapo gharama itakuwa juu ya gharama tajwa hapo juu basi itakupasa kulipia gharama iliyoongezeka.
  • Iwapo vifaa vya mziki na burudani vitaibiwa au kuharibiwa utalipwa si Zaidi ya 500,000/-. Iwapo gharama ya vifaa vilivyoibiwa ni kubwa itakupasa kulipia gharama zilizozidi
  • Iwapo gari lako litavutwa kupelekwa gereji utafidiwa mpaka kiasi cha shilingi 500,000/-

kama gharama zitazidi kiasi tajwa itakupasa kugharamia kiasi kilichozidi.

  • Tathimini: Tunatoa huduma ya ushauri na tathmini bure kwa wateja wanaokata bima kubwa .

 Jambo la kuzingatia: Ni mhimu kujua kwamba iwapo utampa dereva mwingine gari lako, BIMA KUBWA haitahusika na malipo ya fidia kwa dereva huyo pindi atakapopata ajali, ili kuweza kulipwa fidia dereva huyo atapaswa kukata au kukatiwa Bima ya ajali binafsi itakayo mkinga dhidi ya ajali. 

  • Faida na Fidia zifauatazo zitalipwa iwapo utaongeza kiasi cha malipo ya bima :
  • Vurugu au au fujo zinazoweza kuharibu mali yako zitafidiwa iwapo utaongeza malipo ya 0.25% ya thamani ya gari lako. 
  • Vurugu za kisiasa na ugaidi zitafidiwa iwapo utaongeza malipo ya 0.25% ya thamani ya gari lako. 
  • Itakupasa uongeze kiasi cha shilling 50,000/= katika malipo yakoya bima ili uweze kulipwa kwa kushindwa kutumia chombo chako. Utalipwa fidia hii kwa ukomo wa siku 21 ambapo utalipwa kiasi cha shilingi 50,000/= kwa siku.
  • Ili kuepuka makato ya lazima wakati wa fidia (Excess), itakupasa kulipia  10% zaidi ya kiasi unachopaswa kulipia  bima ya gari lako 
  • Mchango wa lazima ni upi? Ni kwanini unatumika kwenye Bima zote za gari?

Kukusaidia uweze kuelewa kwanini makampuni ya Bima yanatoza mchango wa lazima pindi unapopatwa na janga soma Kanuni ya kwanza ya uaminifu ya bima  na  kanuni ya  saba ya Bima  ambayo inazungumzia kupunguza gharama ya upotevu . Hapa kanuni hii inasema pande zote zilizohusika katika bima (Kampuni ya bima na mkata bima) zinatakiwa kufanya biashara katika uaminifu. Hapa inasadikika kwamba mkata bima anatakiwa kuchukua tahadhari zote ili kupunguza uwezekano wa ajali na uharibifu wa mali iliyokatiwa bima . Hivyo basi ili kufanya mkata bima awe na tabia ya uwajibikaji na kutosababisha ajali au uharibifu kiholela itampasa kuchangia kiasi kidogo katika malipo ya fidia atakayolipwa. 

Ni kitu gani hakihusiki katika bima kubwa ya gari binafsi.

Tafadhali tambua ya kwamba yafuatayo hayahusika kwenye sera ya bima yetu ya 

  • Hasara isiyo ya moja kwa moja  (Consequential Loss) inayomaanisha mtu kushindwa kupata kipato kutokana na gari lake kupata ajali na kuharibika. Hasara hii inaweza kulipwa kwa mteja aliyekata bima ya gari la biashara (Motor Commercial)
  • Kushuka kwa thamani, kuisha kwa matumizi ya vifaa, shida katika mfumo wa umeme, breki kuharibika au kuharibika kwa gari kiujumla.
  • Kuharibika kwa tairi , isipokuwa kama uharibifu huo unahusisha ajali na gari nyingine 
  • Kupotea au kuharibika kwa vitu vilivyokuwa vimebebwa na gari 
  • Uharibifu uliotokana na kuzidisha mizigo katika gari lako.

Bonyeza hapa  kujifunza  vitu mhimu  katika bima ya gari:

  • Nifanye nini nipatapo ajali ?
  • Kwanini ni mhimu kufanya tathimini ya gari kabla ya kukata bima?
  • Ni nyaraka zipi  natakiwa kuwa nazo ninapotaka kukata bima  ya gari?
  • Ukitaka kuelewa maswala ya kitalaam juu ya bima hii ya magari binafsi. 

Sasa umeelewa kuhusu sera yetu ya bima ya gari binafsi , iwapo utapenda kupata bima hii tafadhali bonyeza hapa  ili uweze kupata tathmini ya gharama ya bima ya gari lako .unaweza kulipia kwa njia ya mtandao na kujipatia stika yako itakayo tumwa kwako kwa njia ya barua pepe . Iwapo utataka kuongea nasi tafadhali tupigie +255 22 2775039, +255 22 277 4999 au omba kupigiwa kwa ku bonyeza hapa.

 

Kindly note that client login is only available to existing ICEA LION customers
Click here to proceed to the Self Service Portal if you are already a client of ICEA LION.
Otherwise, see products available to buy online