Hii ni bima inayokinga mzigo /bidhaa uliyobeba wakati wa usafirishaji ndani ya nchi kwa njia ya barabara, maji, reli au hata anga. Bima hii inakukinga na uharibifuwa mzigo ambao unaoweza kusababishwa na binadam au ajali itokanayo na majanga ya asili. Bima hii pia inaweza kutoa kinga kwa wahusika wengine watakao husika wakati wa kupakia au kupakua mizigo na mara nyingi kinga hii hutumika kwa usafiri wa reli na barabara. Kama unatumia njia ya maji au anga basi itakupasa upate bima ya mizigo ya aina nyingine (Marine cargo insurance) ili uweze kuwa na kipengele hiki kinachokinga mali yako wakati wa kupakia na kupakua.
Bima hii huanza mara tu mizigo yako inapopakiwa kwenye chombo cha usafiri na kuisha pale mizigo yako inaposhushwa mwisho wa safari. Iwapo itatokea bahati mbaya na mzigo wako usifike mahala husika kutokana na shida iliyojitokeza bima hii itaendelea kukukinga hata pale mzigo wako utakaposhushwa na kupakiwa kwenye chumba kingine cha usafirishaji .
Bima ya usafirishaji wa mizigo ya ndani wakati mwingine hufananishwa na kuchanganywa na Bima ya mizigo (Marine cargo ) sababu ya kufanana kwake katika kutoa kinga ya mizigo yako wakati wa usafirishaji wake. Ukitaka kuielewa zaidi bima hii bonyeza hapa kupata maelezo zaidi Bima ya mizigo
Unaweza kuchagua aina ya bima unayotaka kutoka kwenye maelezo hapo chini:
Kwa kuwa umeshajifunza kuhusu bima hii tafadhali bonyeza hapa kwa manunuzi ya bima hii au tupigie kwenye +255222774999, 2775039 au omba kupigiwa kwa ku bonyeza hapa .
enter your details so we can schedule a call for you
The types of perils covered under this policy are:
Head Office
Plot 331 Kambarage (Rose Garden road) Road, Mikocheni
P.O. Box 1948 Dar Es Salaam
Tel: +255 22 2774999, +255 22 2775039, +255 22 2775059
Fax: +255 22 2775094
E-Mail: insurance@icealion.co.tz
Website: www.icealion.co.tz
Something isn’t Clear?
If you would like to talk to us in person, you can call us on +255 22 277 4999, +255 22 277 5039 or request a call back by clicking here.