BIMA YA BIASHARA
Kama ilivyo kwa mambo mengine,Biashara pia huwa katika hatari ya kukumbwa na majanga mbali mbali , iwapo mfanya biashara hatajikinga na majanga haya anaweza kupata anguko kubwa la kibiashara na kupoteza mali aliyoifanyia kazi kwa muda mrefu. Bima hii ya biashara imebuniwa ili kukuletea ma suluhisho mbalimbali ya bima kutokana na uhitaji wako.Kama kampuni tutatathimini na na kukushauri ni aina gani ya bima itakufaa katika biashara yako.
Faida za bima hii ni zipi?
- Una machaguo mengi ya kipi unataka: Tutakushauri aina ya bima inakayofaa kwa aina ya biashara unayofanya ili kuilinda biashara yako dhidi ya majanga tofauti.
- Tunaweza kukutengenezea kifurushi maalumu : Tuna uwezo wa kukaa na kukubaliana na wewe juu ya kifurushi maalumu cha bima unachokihitaji.kwa ajili ya biashara yako.
- Ni rahisi na uhakika: Unaweza kulipia bima yako kwa machaguo yako uliyochagua na kupewa nyaraka moja iliyorahisishwa maelezo yote ya biashara yako.
- Tuna linda biashara ndogo na za kati(SME): Bima hii itakulinda hata wewe mwenye biashara ndogo ndogo kama duka la vinywaji, duka la nguo, duka la internet, duka la nyama , duka la dawa, maduka ya vinyozi, maduka ya vifaa vya umeme na mengineyo.
Ni vitu gani vya msingi vipo ndani ya bima hii ya biashara?
Bima yetu ya biashara imegawanyika katika vipengengele tofauti amabavyo vinaendana na uhitaji wako mfano, unaweza ukawa hauhitaji kukata bima ya jengo kama wewe ni mpangaji kwenye jengo unalofanyia biashara ,hivyo basi utahitaji kukatia bima vifaa vyako vinavyohamishika katika duka lako pamoja na mali yenyewe.
Unaweza kufanya uchaguzi wako wa nini kikatiwe bima kama ifuatavyo
Kipengele A: Bima ya Moto:
Hii ni bima unayokata kwa ajili ya mali zako ili ikulinde dhidi ya madhara yanasosababishwa na moto na vianzilishi vingine vya majanga. Vianzilishi hivi ni pamoja na moto wenyewe, milipuko, tetemeko la ardhi,milipuko ya volcano, radi, vimbunga ,mafuriko, kupasuka kwa mabomba makubwa, kulipuka kwa matanki ya mafuta, vurugu, majaribio ya silaha kubwa , kuanguka kwa kimondo na moto uliozuka kwenye misitu au mapori.
Mali zinazokatikiwa bima hii ni majengo, vifaa vya ofisi, kompyuta, vifaa/vitu binafsi vya waajiriwa, fedha, mashine na kazi ya Sanaa.
Kipengele B: Bima ya Wizi:
Hii ni bima ambayo itakulipa fidia kutokana na upotevu au uharibifu wa mali uliotokana na vitendo vya wizi/ujambazi uliofanywa kwa kuvunja na kuingia kwenye jengo lako. Ni mhimu kujua kwamba hautalipwa fidia iwapo wizi huu utafanywa na mmoja wa wafanyakazi wa duka/jengo lako au kutokana na wafanyakazi wako kutokuzingatia njia za ulinzi na usalama au uzembe.
Kipengele C: Bima ya vifaa vyote:
Hii ni bima inayokatwa kwa ajili ya mali au vifaa vyote ambavyo havijahusika au kutajwa kwenye kipengele A & B hapo juu.
Vifaa/Vitu vinavyohusika katika katika kipengele hiki ni vile amabavyo vinatumika katika kurahisisha au kufanyia biashara kama kompyuta , printers , na vifaa vingine vinavyoweza kuwa vinapatikana kwenye ofisi au duka.
Ni mhimu kujua kwamba kuharibika kwa kifaa/kitu kulikosababishwa na kuisha kwa matumizi, kushuka thamani, kupatwa na kutu, kuharibika kwa sababu za asili, kifaa/mali kutaifishwa au kufilisiwa na serikali au kuibiwa na mmoja ya wana familia hakutakuwa na ustahili wa kulipwa fidia yeyote.
Kipengele D: Kinga dhidi ya majanga ya kijamii:
Kipengele hiki hukatwa na wafanyabiashara ili kujikinga na madhara yanayoweza kuwapata watu waliokuja katika sehem ya biashara yako ambao wanaweza kukufungulia mashtaka dhidi ya hasara au tatizo lilijojitokeza . matatizo hayo yanaweza kuwa kifo, kuumia ,kupoteza/kuharibikiwa mali au ugonjwa.
Kipengele E: Bima ya Fedha:
Hii ni bima ambayo inakulinda dhidi upotevu wa hela wakati zikipelekwa au kutolewa benki , au ndani ya jengo lako kwa kuibiwa pesa au kuibiwa kwenye kabati ya kuhifadhia pesa. Itambulike ya kwamba bima hii haitalipa fidia kwa matukio yeoyote yanayohusisha ukosefu wa uaminifu wa wafanyakazi, au makosa ya wafanyakazi wa biashara yako .Hii pia ina maana madai yatokanayo na pesa iliyopotea bila ushahidi wa kuibiwa au kuporwa hayatalipwa pia.
Kipengele F: Kinga ya Muajiri:
Hii ni bima inayokatwa na mwajiri kujikinga dhidi ya mashitaka yoyote ya kisheria yanayoweza kuletwa na mfanyakazi wa ndani kutokana na ajali, magonjwa,kifo majeraha yaliyotokea akiwa katika majukumu ya kazi. Iwapo mmiliki kwa bahati mbaya atafariki kipengele hiki kitaendelea kumkinga muwakilishi wa mmiliki kama mke/mume au muwakilishi wa familia iwapo utafunguliwa mashtaka na mtu wa tatu.
Ni kitu gani kingine natakiwa kujua kuhusu bima ya biashara?
- Kwenye kipengele A & B hapo juu, ni mhimu ukaandika na kuweka orodha kamilifu ya vitu vyako vyote na thamani yake pamoja mahala vilipo. Kwenye kipengele C utahitaji kuainisha vifaa ulivyovitaja vitatumika wapi.(kama ni kwenye jengo lako au sehemu nyingine)
- Ili tuweze kuwa na maelezo sahihi ya mali zako na hakikisha unatupa taarifa iwapo utabadili baadhi ya vitu kwenye mkataba na sera yako ya bima ili kuepuka usumbufu wakati wa madai
- Kwenye kupengele cha Bima ya kinga ya kijamii (Kipengele D hapo juu)), itakupasa utoe taarifa iwapo utataka kazi za ujenzi, marekebisho , mafunzo, au matukio mengine ambayo utayafanya nje ya sehemu uliyotaja kama sehemu yako ya biashara ili tuweze kukuingiza kwenye orodha ya biashara za nje ya eneo la kila siku.
- Chini ya kipengele E cha fedha zingatia yafuatayo: Pesa katika kipengele hiki inahusisha , pesa, hundi, warrants, stakabadhi za serikali na nyinginezo.
- Kiasi kinachozidi shs 4,000,000/- ni lazima kiwe chini ya usimamizi wa watu wazima wawili. Ambapo kila mmoja awe amebeba si zaidi ya sh 2,000,000/=
- Kiasi kinachozidi sh 8,000,000/- lazima kisafirishwe na usafiri binafsi. Na lazima kisindikizwe na mtu mzima mmoja ukimtoa dereva wa gari.
Kwakua sasa umeelewa bima yetu ya biashara tafadhali bonyeza hapa kupata maelezo zaidi. Iwapo utataka kuongea na mtoa huduma wetu tupigie kwenye namba +255 22 277 4999, +255 22 277 5039 au omba kupigiwa kwa kubonyeza hapa..