BIMA KWA MAENDELEO NA MAZINGIRA

Kama moja ya makampuni ya pekee kushiriki katika jitihada za umoja wa mataifa  kupitia program yake ya mazingira na uchumi (UNEP –FI) tumejidhihirishia kujitoa na kujitolea kwetu kwenye  maendeleo endelevu na jinsi ya kuilinda dunia .

 Kwa kulinda makampuni na wateja  dhidi yan majanga tunatoa ulinzi na Amani katika uchumi. Tunatengeneza bidhaa zinazowezesha wateja wetu kujikinga dhidi ya hasara inayoweza kuletwa na majanga. Jambo hili linapelekea wateja kutulipa na kuchangia katika uwekezaji wa baadae.Kitendo cha kuwa na ulinzi wa bima kina chagiza ukuaji wa ugunduzi na ujasiliamali kwa kuwa kuna uhakika wa usalama wa kiuchumi.

Ni 2.3% tu  ya watu wanapotumia na kununua bidhaa za bima , hivyo huu ni ushaidi Dhahiri kuwa  wana jamii wengi ambao wako kwenye hatari ya kupoteza mali sababu ya majanga hawana uelewa au hawajafikiwa na huduma ya bima Kupunguza jambo hili tunatengeneza bidhaa ambazo ni rahisi, nafuu na rahisi kuzipata ili tuweze kunyanyua uchumi .

UHUSIKA WETU KATIKA MALENGO YA MAENDELEO

ICEA LION imekuwa ikijihusisha na malengo ya maendeleo ya Umoja wa mataifa (SGDs) has kwenye kupunguza umasikini, kulinda mazingira, na kuhakikisha maendeleo ni kwa wote. Kama watoa huduma ya bima tunatambua mchango wetu katika baadhi ya malengo haya ya umoja wa mataifa .

MCHANGO WETU KWA JAMII

ICEA LION ina nia iliyothabiti ya kulinda kukukuza uzao wa mnyama simba kutokana na ukweli kwamba imeonekana ya kuwa simba wamepungua sana katika mbuga zetu za wanyama hasa nchini Kenya.

ICEA LION ina kampeni yake ya I SEE A LION yaani NAMUONA SIMBA ambayo inauhusiano wa moja kwa moja na jinsi jina letu linavyotamkwa . sisi kama taasisi tunajitahidi kufanya na kuwaza kama wafalme wa mwitu hivyo ilitupasa kuhakikisha tunatoa mchango wetu katika maamuzi ya kulinda ustawi wa simba mbugani.

Kampeni hii imekuwa ikifanywa na ICEA LION kwa kushirikiana na shirika la huduma ya wanyama pori nchini kenya (Kenya wildlife service) ili kukuza uchumi kupitia utalii wa simba.

Tumefanya mambo yafuatayo katika kampeni yetu ya ulinzi na utunzaji wa mnyama Simba:

  • Sensa ya nchi nzima: kwa kushirikiana na Kenya Wildlife Service, tumechangia kiasi cha  shilingi ya kenya milioni  1.28 katika kufanya sense ya majaribio iliyofanyika katika mbuga ya ziwa Nakuru Mwaka 2019 na tumwekeza kiasi cha shilingi ya kenya million  1.7 katika kununua vifaa vya kufanyia sensa hiyo nchi nzima. 
  • Muingiliano wa watu na wanyama: tumewekeza kiasi cha fedha ya kikenya shilingi milioni 12.5  tukishirikiana na wadau waitwao EWASO LIONS na LEWA ili ku wezesha utunzaji na udumishaji wa mahusiano kati ya watu wanaoishi karibu na mbuga za wanyama ili wasaidie katika harakati za kumlinda simba. 

MICHANGO YETU ILIYOGUSA JAMII

  1. EWASO LIONS
  2. KENYA WILDLIFE SERVICE (KWS) Sensa ya simba nchi nzima
  3. KENYA WILDLIFE SERVICE (KWS) Vifaa vya kufanyia sensa
  4. LEWA CONSERVANCY 
  5. LEWA CONSERVANCY – Elimu ya utunzaji wa mbuga na simba
  6. LEWA MARATHON

Our Impact Stories

Bima Ya Biashara

Request a call back Download Brochure BIMA YA BIASHARA Kama ilivyo kwa mambo mengine,Biashara pia huwa katika hatari ya kukumbwa na majanga mbali mbali ,

Read More »
Kindly note that client login is only available to existing ICEA LION customers
Click here to proceed to the Self Service Portal if you are already a client of ICEA LION.
Otherwise, see products available to buy online