Urithi Wetu
ICEA LION Group ni taasisi ambayo inatoa suluhisho la bidhaa na huduma bora za bima , pensheni na mifuko ya hifadhi . Taasisi hii ilianzishwa baada ya mabadiliko yaliyofanyika kati ya kampuni ya Kenya insurance Company Limited na Insurance Company of East africa (ICEA) Mwaka 2012 na kupelekea kupatikana kwa jina la ICEA LION.
Mizizi ya ICEA LION inatokea miaka ya 1895 ambapo taasisi hii imekuwa ikitoa huduma hizi za kifedha , kwa miongo mingi tumekuwa tukilinda mali na kutengeneza fursa za kupata mali hapa afrika mashariki. Katika dunia ya sasa inayobadilika kwa kasi tumekuwa tuki zingatia bidhaa zinazoenda na wakati na kuzingatia mahitaji tofauti ya walteja wetu.
