Hii ni bima ya mizigo inayokulinda dhidi ya hasara au uharibifu utakaotokea kwa bidhaa zako zikiwa njiani kutoka kwa muuzaji kuja kwako. Mzigo huu utasafirishwa kwa njia ya maji ingawa sera yetu inaweza pia kulinda mzigo wako wakati ukisafirishwa kwenda au kutoka bandari kwa kupitia barabara, reli, anaga au hata njia za maji zilizopo ndani ya nchi. Pia tuna uwezo wa kukukatia bima itakayokulinda kutoka sehemu ulipotolewa mzigo mpaka mahala mzigo utakapohifadhiwa . Bima hii hujulikana kama Bohari kwa Bohari (warehouse to warehouse) Kwa ujumla , tunakulinda dhidi ya hasara au uharibifu wowote utakaotokea kwenye mizigo au shida yoyote itakayotokea wakati wa usafirishaji.Unaweza kununua bima yetu ya mizigo kwa njia ya hapa. Mhimu: Pia tunatoa bima inayotoa kinga dhidi ya chombo cha usafiri majini Marine Hull Insurance. Hii ni bima inayokatwa maalumu kwa ajili ya chombo chako (Meli) ,bima hii haihusishi injini ya meli na baadhi ya vifaa ambatanishi kama masts, na rigging . Kujua zaidi kuhusu bima hii bonyeza hapa
Hiki ndio kifungu kipana chenye kuchukua majanga yote yasababishayo uharibifu au upotevu wa mali isipokuwa yale tu yaliyotengwa kwa mujibu wa makubaliano.
Hiki ni kifungu ambacho hukinga dhidi ya majanga maalumu ambayo mteja ametaka kujikinga nayo. Kifungu hiki hutoa bima ile ya msingi na kuacha vitu vingine vinavyopatikana kwenye kifungu.
Hiki ni kifungu ambacho bima inatoa kinga kwa majanga yaliyochaguliwa pekee.
Tembelea msingi wetu wa Maarifa ili kupata habari kamili juu ya aina zetu za vifuniko
Head Office
Plot 331 Kambarage (Rose Garden road) Road, Mikocheni
P.O. Box 1948 Dar Es Salaam
Tel: +255 22 2774999, +255 22 2775039, +255 22 2775059
Fax: +255 22 2775094
E-Mail: insurance@icealion.co.tz
Website: www.icealion.co.tz
Something isn’t Clear?
If you would like to talk to us in person, you can call us on +255 22 277 4999, +255 22 277 5039 or request a call back by clicking here.