BIMA YA AJALI BINAFSI
Bima ya ajali binafsi ni nini?
Bima ya ajali binafsi ni ile ambayo inatoa fidia kwa mtu ambaye amepatwa na majeraha, ulemavu au kifo .ni bima ambayo pia inafidia gharama za matibabu zilizojitokeza kutokana na ajali, kwahiyo bima hii huwa kama nyongeza kwa bima yako ya maisha au bima ya matibabu. Kiasi utakacholipia kitategemea na vigezo vya bima utakayotaka kuchukua hivyo fidia utakayolipwa itategemea pia kipato chako cha kila siku. Bima hiiinatumika iwapo utapata ajali mahali popote duniani.
Bima ya ajli ya kikundi: hii ni bima dhidi ya ajali ambayo inakatwa kwa ajili ya kundi la wafanyakazi, familia, waajiriwa, vyuo, vikundi vya maendeleo au kikundi chochote ambacho kina watu wenye kazi/dhumuni au matakwa yanayofanana
Vitu vya msingi vilivyopo katika bima ya ajali binafsi kutoka ICEALION
- Kifo: Tutamlipa mhusika uliyemtaja kwenye makubaliano au aliyeteuliwa au kuidhinishwa kama msimamizi wa mirathi yako kiasi cha mishahara ya mda uliokubalika kutokana na kifo kilichosababishwa na ajali..
- Ulemavu wa kudumu : Tutakulipa fidia asilimia ya kiwango kilichokubaliwa katika makubaliano ya bima hii au jumla ya mishahara iliyokubaliwa kwa ajili ya ulemavu wa kudumu .
- Malipo ya week (Ulemavu wa muda ): Fao hili litakulipa malipo ya wiki iwapo utakuwa umepata ajali iliyosababisha kupoteza uwezo wako wa uzalishaji mali kwa mda .Malipo haya ni ya muda mfupi mpaka utakapokuwa umepona. Ukomo wa juu kabisa wa malipo haya ni wiki 104
- Gharama za matibabu: Tutakurudishia gharama za matibabu ulizolipia ikiwa ni pamoja na huduma ya macho na meno ambayo imetokana na ajali . Huduma hii ina ukomo maalumu.
- Uokoaji wa dharura: ICEALION itagharamia gharama zote za uokoaji katika kupata msaada wa kitabibu baada ya ajali.
- Vifaa vya msaada wa ulemavu: ICEALION italipia gharama ya vifaa vya usikivu,upumuaji,magongo au vifaa vingine vinavyohitajika katika kujiuguza.
- Gharama za kurudisha mwili: Iwapo utapoteza maisha, ICEALION itagharamia gharama zote za usafirishaji mwili mpaka mahali unapoishi..
- Gharama za mazishi: ICEALION, Italipa gharama za mazishi kama zilizovyoanishwa kwenye makubaliano ya awali kabla kupatwa na umauti uliosababishwa na ajali.
Kitu gani kingine natakiwa kujua kuhusu Bima ya ajali kutoka ICEALION?
- Bima binafsi ya ajali ni tofauti na bima ya matibabu: Bima ya matibabu iliyoko kwenye Bima hii ya ajali ni maalumu kwa ajali , haiusiani na gharama za matibabu mengine yatokanayo na magonjwa mengine.
- Ni vyema kujua kwamba bima hii inaweza kuwa nyongeza kwa bima yako ya matibabu uliyonayo. Iwapo hautakuwa na bima ya matibabu basi bima hii ya ajali itakusaidia moja kwa moja..
- Shughuli zenye hatari: Bima hii haitalipa madai kwa ajali ambayo imetokea kutokana na shughuli zenye hatari . shughuli za hatari zilizoainishwa kwenye sera yetu ni pamoja na mbio za magari, mbio za farasi, michezo ya kwenye barafu, upandaji wa milima mirefu. Ingawa unaweza kupata bima za shughuli au michezo hatarishi kwa kulipia gharama zaidi kwa huduma hizi za kipekee. Tafadhali piga kwenye namba zetu kujua Zaidi.
- Wafanyakazi wa Usafiri wa anga: Iwapo unafanya kazi kwenye shirika la ndege na kwabahati mbaya ukapata ajali ukiwa kazini bima hii haitahusika . Hii ni kwa sababu tayari utakuwa umekatiwa bima na kampuni yako ya usafiri wa anga kwa ajili ya ajali.
- Matatizo ya akili: Hatutaweza kulipa madai yantokanayo na ajali kwa mtu mwenye matatizo ya afya ya akili.
- Matatizo ya uzazi: Iwapo mteja atapatwa na matatizo ya uzazi au shida ya kujifungua kufatia ajali aliyoipata ICEALION haitahusika katika madai haya.
- Kujiua au kujiweka katika mazingira hatarishi: iwapo umejiweka kwenye mazingira hatarishi kwa makusudi (isipokuwa katika kujaribu kuokoa maisha ya mtu) au kutaka kujiua ICEALION haitalipa madai hayo..
- Uwendawazimu: Iwapo utapata majeraha kutokana na uwendawazimu au kuchanganyikiwa kwa akili, ICEALION haitahusika na malipo ya madai hayo.
- Vita na ugaidi: ICEALION haitaweza kulipa madai yeyote ya ajali inayohusisha vita ,ugaidi, mapinduzi,vurugu za kisiasa au mapinduzi.
Iwapo utahitaji kujikinga dhidi ya majanga hayo tafadhali tupigie kwenye mawasiliano yaliyopo hapo chini kujua Zaidi.
BIMA YA AJALI YA KIKUNDI
ICEALION pia tunatoa bima ya ajali kwa vikundi maalumu kama vyama vya wanafunzi, waajiriwa na wafanyakazi
Bima ya ajali ya kikundi hutolewa kwenye nyaraka moja yenye sera za bima hiyo kwa ajili ya kikundi husika na mara nyingi huchukuliwa na mashirika au waajiri kama sehemu ya fao kwa wafanyakazi pindi kinapotokea kifo , ulemavu wa muda na ulemavu kudumu .hapa fidia hizi hulipwa kwa mwajiriwa au wategemezi wakee. Gharama za matibabu hulipwa pia kwa mtu aliyepata ulemavu wa mda.
Bima hii huuzwa kwa kuzingatia mahitaji maalumu ya kikundi hivyo unahitaji kuwasiliana nasi ili tuweze kukupa muongozo ulio sahihi.
Sasa umeelewa juu ya Bima ya ajali kutoka ICEA LION, Iwapo utahitaji kupata bima hii tafadhali bonyeza hapa au tupigie kwenye+255 22 277 4999, +255 22 277 5039 au omba kupigiwa kwa kubonyeza hapa..