BIMA YA SAFARI

Bima ya Safari ni nini? 

Hii ni bima inayokulinda dhidi majanga ya kiuchumi, upotevu au uharibifu unaoweza kutokea ukiwa umesafiri nje ya nchi. Bima hii inaweza kukupa fidia ya  kucheleweshwa kwa vifurushi au mzigo wako,msaada wa kisheria kwa matukio kama kughairishwa au kufutwa  kwa safari katika dakika za mwisho, matibabu  dharura safarini.

Unaweza kuchukua bima ya safari fupi au safari ndefu za kimataifa na ni bima ya hiari ingawa kuna baadhi ya nchi ni lazima uwe na bima hii ili kuweza kwenda kwenye inchi hizo 

Bonyeza hapa kununua bima yetu ya safari na upate barua ya maobi ya visa ndani ya dakika moja.

Kwanini nahitaji bima hii ya safari?

Inashauriwa ya kwamba mtu anapotaka kusafiri ni vyema kupata bima hii bila kujali ni kwa hiari au ni kwa mujibu wa sheria ya nchi unayokwenda .Bima hii ni ya gharama nafuu na itakupa Amani ya moyo ukiwa safarini .

Matukio yatakayokufanya uhitaji kuwa na bima ya safari ni pamoja  na:

  • Safari yako ikisitishwa ghafla na mtoa huduma. 
  • Safari yako imecheleweshwa na kusababisha kukosa ndege nyingine ambayo ungepanda ili kuunganisha 
  • Unahitaji msaada wa kisheria ukiwa nje ya nchi
  • Mizigo yako imecheleweshwa
  • Mizigo yako imepotea
  • Unahitaji msaada wa matibabu
  • Iwapo utafariki ukiwa safarini
  • Iwapo ni kwa mujibu wa sheria ya nchi unayokwenda 
  • Iwapo umevamiwa na kupoteza fedha na nyaraka za 
  • Unahitaji ushauri wa kitaalam kutoka kwa wataalam wa maswala ya safari. 

Faida za Bima ya Safari?

Faida  Bima 
1 Gharama za matibabu ya dharura ICEA LION itakurudishia gharama za matibabu ya dharura  uliyofanya kutokana na majeraha au ugonjwa ulioupata ukiwa safarini kwenda nje ya nchi au ukiwa safarini kuja Tanzania
2 Muendelezo wa matibabu ukiwa  Tanzania ICEA LION italipia gharama ulizopata kwa mujibu wa faida za bima hii kama zilivyoainishwa. Hii ni pamoja na muendelezo wa matibabu ya ugonjwa au majeraha yakiyo ambayo matibabu yake yalianzia ukiwa nje ya nchi.

Matibabu haya ni lazima yafanywe ndani ya siku 30 toka ulipoingia Tanznaia  

3 Matibabu yatakayohitaji kusafirishwa kwenda mahala pengine. I wapo utaumwa au kupata jeraha ambayo imeanishwa kwenye bima hii na itahitajika kusafirishwa kwenda mahala pengine au kurudishwa  nchini Tanzanaia ICEA LION italipa gharama hizo ikiwa ni pamoja na gharama za wauguzi waliokusindikiza.
4 Ufanikishaji wa safari kwa mwanafamilia atakayekusindikiza  iwapo utaumwa au kupatwa na kifo. Iwapo utalazwa kutokana na ugonjwa wa ghafla au kutokana na ajali kwa zaidi ya siku 20 au iwapo utapatwa na kifo ICEA LION itamgharamia mwanafamilia ambaye amekusindikiza na ambaye ni mkazi wa Tanzania. Hii ni iwapo mwanafamilia huyu hawezi kusafiri kwa gharama zake. 
5 Safari ya mtu wa karibu. Iwapo wakati wa safari yako iliyokatiwa bima utapatwa na ugonjwa au majeraha ICEA LION itakulipa kiasi cha ziada kitakachokidhi mahitaji ya kusafiri na malazi  ya mtu atakayesafiri , kukaa na wewe au kusafiri na wewe wakati wa kurudi Tanzania.

Swala hili litafanywa kwa kuzingatia ushauri wa kidaktari uliotolewa na wataalam wa afya na kwa kuzingatia makubaliano ya kimaandishi yaliyoandikwa baina ya mteja na ICEA LION

6 Kurudishwa kwa mwili / Gharama za mazishi  Iwapo itatokea bahati mbaya ukapoteza maisha ,ICEA LION italipia gharama za kurudisha mwili wako nchini Tanzania au kugharamia gharama za mazishi iwapo mwili utazikwa mahali mauti yalikotokea
7 Kurudi Nyumbani baada ya kupata taarifa za msiba wa mtu wa karibu wa familia . Iwapo itakubidi ukatize safari yako kutokana na kifo cha mtu wa karibu wa familia, ICEA LION itagharamia gharama za kukurudisha nyumbani iwapo umeshindwa kusafiri kwa njia zako binafsi, gharama hizi zitalipwa baada ya kuwasilisha nyaraka husika wakati wa madai. 

 

8 Huduma ya dharura ya Meno Iwapo utahitaji huduma ya dharura ya meno wakati wa safari kwa ajili kupata nafuu kutokana na maumivu yaliyojitokeza ghafla , ICEA LION  itakurudishia gharama ulizotumia katika kupata dawa,jeraha au  kungóa jino/meno.

Gharama hizi zitarudishwa iwapo mhusika atawasilisha nyaraka mhimu atakazoombwa wakati wa madai .kwahiyo ni mhimu kujua nyaraka na viambatanisho vinavyotolewa kabla na wakati wa safari .Bonyeza hapa kupitia vitu vya kuzingatia na kuambatisha unapotaka kufanya madai..

9 Manufaa ya kila siku Hospitalini. Iwapo utakuwa nje ya nchi na ikakubidi ulazwe hopitalini kwa Zaidi ya saa 24  mfululizo, ICEA LION italipa gharama za kulazwa kwa kila masaa 24 uliyolazwa kwa kufuata kiasi mahususi kilichotajwa na kuoneshwa kwenye nyaraka yetu ya sera za bima hii 
10 Bima dhidi ya ajali binafsi. Iwapo kwa bahati mbaya utapata ajali iyakayokusababishia ulemavu au hata kifo kutokana na majeraha uliyoyapata ukiwa safarini, ICEA LION itakulipa mafao yako ya bima kwa kufuata kiasi kilichotajwa kwenye nyaraka yenye za sera bima hii. 
11 Huduma ya Msaada Iwapo utapatwa na dharura ya kiafya au dharura nyingine ICEA LION itafanya utaratibu ufuatao kwa kufata vigezo na masharti ikiwemo ruhusa, usitishwaji, na umuhimu katika sera husika na sheria husika. 

Malipo ya Fedha 

Iwapo umeibiwa , kupoteza , majeraha au ugonjwa  wakati wa safari na unahitaji fedha ya kulipia safari au malazi ,ICEA LION itakushauri wewe au muwakilishi wako juu ya utaratibu wa  kupewa malipo ya awali ya nyongeza ambayo yatarejeshwa yakiwa na tozo la 10% Zaidi kama ada ya uwezeshaji. 

Msaada wa kibalozi 

Ikiwezekana, ICEALION itakupa maelezo na maelekezo sahihi ya jinsi ya kupata msaada kutoka ofisi ya ubalozi wa nchi yako iliyopo kwenye nchi uliyofikia

Safari ya dharura na malazi

Ikiwezekana, ICEA LION itakupa msaada wa kukuandalia usafiri mwingine wa dharura na malazi . 

Ujumbe wa dharura 

ICEA LION watatuma ujumbe wa dharura kwa niaba yako  kwenda kwa mtu unayetaka apate ujumbe huo iwapo safari itacheleweshwa, utapatwa na ugonjwa au majeraha.

12 Gharama za kazi za kisheria ukiwa nje ya nchi. ICEA LION itakurudishia gharama ambazo zimeoneshwa kwenye faida ya bima hii ambapo tutakurudishia gharama zote utakazopata kutokana na shughuli za kisheria wakati wa kufatilia haki, malipo au fidia dhidi ya mtu wa tatu ambaye  anakudai kutokana na majeraha au kifo kilichotokea wakati bima yako ikiwa hai. 
13 Shambulio   ICEA LION itakulipa kwa kila saa 24 ambazo utakuwa ukipata matibabu ( Yaliyoainishwa katika kipengele namba 1- matumizi ya dharura) kutokana na shambulio ulilopata ukiwa safarini..  
14 Kusitishwa kwa safari au kupunguzwa kwa safari kutokana na hali mbaya iliyojitokeza  ICEA LION itakurejeshea kiasi cha fedha kwa gharama  iliyojitokeza  baada ya safari kusitishwa au kufupishwa kutokana na yafuatayo

  • Kifo cha ghafla , majeraha au ugonjwa kwako au mke,mtoto ,ndugu au mfamyakazi/biashara mwenzio.
  • Majanga ya asili kama radi,kimbunga ,tetemeko na mafuriko.
15 Upotevu wa mizigo ICEA LION itakurejeshea gharama utakazoingia kutokana na kupotea kwa mzigo , au baadhi ya vitu katika mzigo wako  au kupelekwa sehemu nyingine kimakosa kwa Zaidi ya saa 6.
16 Kucheleweshwa 

kwa safari

ICEA LION itakulipa gharama utakazoingia kutokana na kucheleweshwa kwa safari kwa Zaidi ya masaa 6. kuchelewa huku kunaweza kuwa ni matokeo ya kupotea kwa nyaraka ,ajali,kuchelewa kwa usafiri wa barabara au reli au bahari uliochelewa kutokana na matatizo ya hali ya hewa,au kuharibika kwa chombo husika cha usafiri. 
17 Kurejeshewa gharama ya usafiri na malazi kutokana na kuchelewa safari.  Iwapo utashindwa kufika katika mda sahihi wa kuondoka katika nchi husika kurudi nchini kutokana na kuharibika kwa usafiri uliokuwa ukikupeleka uwanja wa ndege kuharibika,ICEALION itakurudishia kiasi cha fedha kama ilivyo ainishwa kwenye jedwali la faida za bima hii..

Ni mhimu kujua kwamba malipo haya yatafanywa kwa kuzingatia gharama za makubaliano ya safari ya awali. Gharama zitakazokuwa mpya kutokana na kubadili daraja la usafiri hazitahusika. 

18 Kinga ya kisheria dhidi ya watu wengine. ICEA LION itakupa kinga dhidi ya mtu mwingne anayeweza kukushitaki au kudai fidia kutokana majeraha au uharibifu wa mali uliosababishwa na wewe
19 Kutekwa Iwapo kwa bahati mbaya ndege itatekwa au kuwekwa kizuizini kwa ndege au wahudumu wa ndege au chombo unachosafiria ,ICEA LION itakulipa kiasi cha dola 100 kwa kila masaa 12 ambayo utakuwa umetekwa au kuwa kizuizini kama ilivyoainishwa kwenye sera na faida za bima hii.

Ni mhimu kujua kwamba itakupasa uwe na nyaraka ya maandishi kutoka kwa msafirishaji kuhusu tukio hili ili uweze kuwasilisha  madai yako.   

 

20 Dhamana Iwapo utafungwa au kushikiliwa na vyombo vya dola ukiwa nje ya nchi, ICEA LION italipa gharama ya kiasi kilichotajwa kwenye sera yetu ya safari kwa ajili ya kukudhamini  kama kifungo hicho kinatokana na sababu zisizo za kimakusudi za kuvunja sheria au miongozo ya nchi uliyotembelea .

Itambulike ya kwamba tampasa mteja kurudisha kiasi cha gharama tajwa hapo juu kwenda kwa ICEALION ndani ya siku 30 toka kuachiwa. 

21 Upotevu wa hati ya kusafiria  Iwapo utapoteza hati ya kusafiria ukiwa nje ya nchi, ICEALION itakulipa gharama zote utakazoingia katika kupata hati mpya.

Kiasi hiki ni kwa mujibu wa kiasi kilichotajwa kwenye faida za bima hii.

22 Matukio maalumu Iwapo itatokea ukacheleweshwa katika matukio mhimu ambayo hayawezi kughairishwa, ICEALION itakurejeshea gharama zilizozidi sababu ya kutumia usafiri mbadala au kuongeza malipo kwa ajili kufanikisha kufika kwenye tukio maalum kama ilivyopangwa. urejeshwaji huu wa gharama utakuwa kwa mujibu wa kikomo cha kiasi tajwa katika sera na faida za bima hii…

Kitu gani kingine natakiwa kujua kuhusu Bima ya Safari? 

Unaweza kuongeza fao la kinga dhidi ya UGAIDI kwenye bima yako ya safari  kwa kuongeza kiasi kidogo cha fedha kwenye malipo. Hapa utapata matibabu ya dharura  na ajali inayoweza kukupata kutokana na matukio ya kigaidi.

Hii pia inaweza kupatikana kwenye bima yako ya safari iwapo utakuwa umechukua kipengele cha matibabu na ajali binafsi 

Tafadhali tambua ya kwamba maelezo yote juu ya faida ya bima hii yapo katika nyaraka ya sera za bima yetu , yakupasa kusoma na kuelewa faida na kinga  za bima hii kabla ya kusafiri. 

Intana Specialty Assistance Team hawa ni wataalam  ambao namba zao zipo kwenye kadi ya dharura utakayopewa . unatakiwa kuwasiliana na wataalamu hawa mara tu unapokuwa unahitaji huduma ya kiafya au baada ya kupata ajali. 

Piga namba hizo pia iwapo kitatokea kifo cha mtu mwenye bima yetu  hivyo ni mhimu kuhakikisha kuna mtu mwingine mwenye namba hizo za wataalam.

Ni mhimu kujua ya kwanza ICEALION haitahusika na gharama zozote zitakafikiwa bila kuidhinishwa na wataaam wa Intana.

Kadi ya dharura huwa na mawasiliano na namba za dharura tu na haitumiki kama kadi ya matibabu

Iwapo utataka kuchukua Bima yetu ya safari , tunakukumbusha kuangalia vigezo vyote na mahitaji ya bima hii kabla ya kusafiri. Iwapo hautawasilisha maelezo yaliyotimia itachangia katika kuchelewa kwa mchakato wa madai. Bonyeza hapa kuweza kuona vigezo vyetu vya jinsi na vigezo vya kuwasilisha  madai.

Sasa umeelewa Bima ya safari ni nini, bonyeza hapa  kuweza kujipatia Bima yako ya safari kutoka ICEA LION tupigie +255 22 277 4999, +255 22 277 5039 au omba kupigiwa kwa ku bonyeza hapa  

Kindly note that client login is only available to existing ICEA LION customers
Click here to proceed to the Self Service Portal if you are already a client of ICEA LION.
Otherwise, see products available to buy online